Kocha wa Croatia ajiuzulu baada ya timu kutolewa kombe la dunia
Eric Buyanza
July 8, 2026
Share :

Shirikisho la Soka la Croatia limetangaza kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa, Zlatko Dalić, amejiuzulu wadhifa wake kufuatia kuondolewa kwa Croatia katika Kombe la Dunia.
Dalić mwenye umri wa miaka 59 aliteuliwa kuinoa Croatia mwezi Oktoba mwaka 2017 na anamaliza kipindi chake cha karibu miaka tisa baada ya timu hiyo kufungwa na Ureno katika hatua ya 32 bora ya mashindano.
Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye akaunti rasmi ya Shirikisho la Soka la Croatia katika mtandao wa X, shirikisho hilo lilimpongeza Dalić kwa mchango wake mkubwa katika mafanikio ya timu ya taifa.
"Alifika kwa unyenyekevu. Alikuwa na safari isiyosahaulika. Anaondoka kwa heshima. Baada ya karibu miaka tisa, kocha mkuu Zlatko Dalić ameamua kufunga ukurasa wa kipindi chake chenye mafanikio makubwa akiwa na Croatia," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.





