Kocha wa Mayele na Inonga adai mishahara Congo
Sisti Herman
June 25, 2024
Share :
Kocha wa timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Sébastien Desabre, ameripotiwa kudai mishahara yake ambayo hajalipwa na Serikali ya Congo.
Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari, Kocha huyo wa zamani wa Uganda hakupokea stahiki zake kwa robo ya mwisho na ile ya sasa kwa sababu ambazo bado hazijajulikana hadi sasa.
Hali inaweza kumsukuma kuwasilisha malalamiko kwenye kamati ya usuluhishi wa migogoro ya shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA).
Kocha Sébastien Desabre tayari ameongeza mkataba ambao unamfunga kusalia ndani ya timu ya taifa hadi 2029.
Tangu kuteuliwa kwake (DRC), kocha huyo wa zamani wa Esperance de Tunis ameshiriki katika mechi 23 na rekodi ya ushindi 9, sare 8 na kushindwa 6.