pmbet

Kocha wa Morocco alikataa bao la Mbappe alilowafunga.

Joyce Shedrack

July 10, 2026
Share :

Kocha mkuu wa Morocco Mohamed Ouahbi ameonyesha kutoridhishwa na maamuzi ya mwamuzi baada ya timu yake kuondolewa katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia kufuatia kufungwa mabao 2-0 na Ufaransa mjini Boston.

 

Ouahbi amedai kuwa bao la kwanza la Ufaransa halikupaswa kuruhusiwa kwa sababu lilitanguliwa na tukio la mpira kugusa mkono wa kiungo wa Ufaransa, Adrien Rabiot kabla ya Kylian Mbappe kufunga.

World Cup news: Kylian Mbappe shuts down injury concern after Morocco clash

Morocco ilikuwa imeanza vizuri mchezo huo huku kipa Yassine Bounou akiokoa penalti ya Mbappe katika kipindi cha kwanza. Hata hivyo, Mbappe aliifungia Ufaransa bao la kwanza dakika ya 60, kabla ya Ousmane Dembele kuongeza la pili dakika sita baadaye na kuipa Les Bleus ushindi uliowapeleka nusu fainali.

 

Akizungumza na beIN Sports Ouahbi alisema tukio lililozaa bao la kwanza liliwachanganya wachezaji wake kwa kuwa wengi waliona kulikuwa na mpira wa mkono.

 

"Bao lilitokana na mpira wa kugombea baadhi ya wachezaji walisimama kwa sababu waliona kulikuwa na mpira wa mkono ilikuwa ni handball, lakini sijui kama ilipaswa kuamuliwa au la, sijui," amesema Ouahbi.

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet