Kocha wa Prisons atimuliwa siku chache baada ya kipigo cha Simba.
Joyce Shedrack
February 25, 2026
Share :
Klabu ya Tanzania Prisons imetangaza kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu, Zedeckia Evans Otieno kwa makubaliano ya pande zote mbili kufuatia mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo iliyopo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi kuu bara.
“Uongozi wa Tanzania Prisons Football Club unamshukuru Kocha Otieno kwa mchango na huduma yake kwa kipindi chote alichoitumikia timu na unamtakia kila la heri katika majukumu yake.” imesema sehemu ya taarifa rasmi ya klabu hiyo kwa umma.





