Kocha wa Real Madrid anaamini Remontada ugenini dhidi ya Bayern.
Joyce Shedrack
April 11, 2026
Share :
Kocha wa Real Madrid Álvaro Arbeloa baada ya kupata sare kwenye mchezo wa usiku wa jana wa Laliga dhidi ya Gerona amezungumzia mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich utakaochezwa Ujerumani utaochezwa Jumatono ya April 15.

Arbeloa ambaye hajapata matokeo ya ushindi akiiongoza Madrid katika michezo mitatu mfululizo iliyopita amesema anaamini wanaweza kulipiza kisasi ugenini na kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
“Itakuwa vita nina uhakika tutaenda Munich tukiwa na 𝐔𝐇𝐀𝐊𝐈𝐊𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐀”
“Jumatano utakuwa 𝐮𝐬𝐢𝐤𝐮 𝐰𝐞𝐭𝐮 dhidi ya Bayern, kurejea (remontada) kunawezekana tutatoa nguvu zetu kwa asilimia 200 kwa hilo kama kuna timu moja inayoweza kushinda kule, ni 𝐑𝐄𝐀𝐋 𝐌𝐀𝐃𝐑𝐈𝐃.”Amesema Arbeloa.
Real Madrid ilipoteza mchezo wa kwanza wa robo fainali dhidi ya Bayern Munich wakiwa nyumbani kwa magoli 2-1.





