Kocha wa Simba atua ES Tunis
Sisti Herman
October 4, 2026
Share :

Baada ya kupata mafankio kwenye nchi mbalimbali kama Tanzania na Morocco, aliyekuwa kocha wa klabu ya Simba Pablo Franco Matrin amejiunga na timu ya Esperanse Sportive De Tunis ya nchini Tunisia akitokea MAS FEZ ya Morocco.
Kocha huyo aliyeisaidia Mas FEZ kuwa Mabingwa wa Morocco msimu uliopita wa ligi kuu soka nchini Morocco amejiunga na ES Tunis kwaajili ya kuirudisha timu hiyo kwenye ramani ya timu tishio barani Afrika kama ilivyo kawaida yao.





