Kocha wa Simba awatisha KMC kuelekea mchezo wa kesho.
Joyce Shedrack
February 10, 2026
Share :
Kocha wa Mkuu wa Klabu ya Simba Steven Barker amesema, anahitaji ushindi katika mechi ya kesho ili aweze kusogea juu kwenye msimamo wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
Barker amezungumza hayo leo Februari 10, 2026 alipokuwa akizungumzia maandalizi ya mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC mara baada ya kutoka katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika nchini Angola dhidi ya Petro Atletico waliotoka sare ya bao 1-1.
Kocha huyo amesema hakuna mchezo rahisi kwenye Ligi Kuu huku akisema kila mechi kwao ni muhimu kupambana kupata matokeo ya ushindi ili wapate alama tatu.





