Kocha wa Yanga aishtaki Angola FIFA.
Joyce Shedrack
March 13, 2026
Share :
Taarifa kutoka kwa mwandishi mkubwa wa habari za michezo Afrika raia wa Ghana @mickjnr zimeripoti kuwa Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Gonçalves amewasilisha kesi dhidi ya Shirikisho la Soka la Angola kwa Shirikisho la Soka Duniani FIFA.
Inaelezwa kuwa shirikisho hilo bado linamchukulia kama kocha wao kikataba, huku baadhi ya masharti muhimu ya mkataba wake yakidaiwa kutotekelezwa tangu alipoondoka.
Chanzo kilicho karibu na suala hilo kimesema:
“Kocha alijaribu kwa muda mrefu kuepuka kwenda FIFA, lakini hakukuwa na chaguo lingine kutokana na kutotekelezwa kwa makubaliano na kukosekana kwa majibu kuhusu namna walivyopanga kutatua tatizo hilo.”.





