Kocha wa Yanga akiri ana imani kubwa na wachezaji wake.
Joyce Shedrack
August 11, 2026
Share :
Kocha Mkuu Yanga Manqoba Mngqithi amezungumza kuelekea mchezo wa kesho wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga akiweka wazi kuwa anatamani kuona kitakachotokea.
"Habari za asubuhi kwa wote. Hii ni mara yangu ya kwanza kushiriki katika Derby hii, hivyo nina hamu kubwa ya kuona kitakachotokea.
“Maandalizi yetu yamekwenda vizuri, ingawa hatukupata muda mrefu wa kujiandaa kwa sababu timu zote mbili zilikuwa na michezo mwishoni mwa wiki. Pia hatukupata muda wa kutosha wa maandalizi wakati wa kipindi cha kabla ya msimu kuanza. Hata hivyo, naamini hali hiyo ni sawa pia kwa Simba”.
"Kwa hiyo itakuwa jambo la kuvutia kuona namna timu zote mbili zitakavyocheza. Nina imani kubwa na timu yangu. Tuna kikosi chenye uwezo wa kucheza soka zuri na la kuvutia" Kocha Mkuu @manqoba.mngqithi





