pmbet

Kocha wa Yanga alia na ubovu wa viwanja.

Joyce Shedrack

March 20, 2026
Share :

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga raia wa Ureno Pedro Concalves, amesema ratiba yao ya michezo ya ugenini imekuwa migumu kutokana na ubora wa viwanja vya Mikoani. 

 

"Jambo lingine muhimu ni ubora wa viwanja. Kuna tofauti kubwa unapocheza kwenye uwanja wenye ubora mzuri na ule usio na hali nzuri. Katika baadhi ya michezo ikiwemo wa mwisho, timu zote zilipata ugumu kutokana na hali ya uwanja jambo lililoathiri umakini na umaliziaji.

“Katika michezo yetu ya hivi karibuni mingi imekuwa ya ugenini mara nyingi katika mazingira magumu. Mfano mzuri wa kiwango chetu ugenini ulikuwa mchezo wa Singida, ambapo tulicheza kwenye uwanja mzuri uliotuwezesha kucheza soka bora zaidi”.

“Ikiwa tunataka kuinua kiwango cha soka ni muhimu pia kuboresha viwanja. Hata hivyo, tunapaswa kuendana na hali na kutafuta njia za kuwazidi wapinzani wetu”.

"Pamoja na changamoto zote, tunaendelea kuwa na mtazamo chanya. Tuko kileleni mwa ligi na tunaamini bado tuna nafasi kubwa ya kuboresha kiwango chetu. Kesho, lengo letu ni kutengeneza nafasi nyingi zaidi, kuwa makini katika umaliziaji na kupigania pointi tatu"Amesema kocha wa Yanga.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet