Kocha wa Yanga ashinda tuzo ya kocha bora wa mwezi April.
Joyce Shedrack
May 13, 2026
Share :
Aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa ligi kuu kwa mwezi April.

Pedro aliyeingia fainali na Steve Barker wa Simba na Etiene Ndairagije wa TRA United, aliiongoza Young Africans kushinda michezo yote mitatu iliyocheza mwezi huo na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi, ikifunga mabao 12 na haikuruhusu bao.
Young Africans ilizifunga Tanzania Prisons (3-0), Mbeya City (6-0) na Pamba Jiji (0-3).





