Kocha wa Yanga atamani kucheza na mashabiki dhidi ya FAR Rabat.
Joyce Shedrack
February 6, 2026
Share :
Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema aangetamani kucheza mchezo wa kesho dhidi ya FAR Rabat kukiwa na mashabiki jukwaani ila wanalazimika kucheza mchezo huo bila mashabiki.
Akizungumza kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya AS FAR ya Morocco na Yanga unaotarajiwa kuchezwa kesho Jumamosi majira ya saa 4:00 usiku nchini Morocco, Goncalves amesema si vyema kucheza majukwaa yakiwa matupu.
“Tungefurahi kucheza mbele ya mashabik, Si vyema kucheza kwenye majukwaa matupu kwani tunahitaji sana mpira uchezwe kwenye Hali yake lakini imetokea hivyo,Tutacheza hivyo na nilicheza hivyo hapo Agadir,Najua ilivyo hali wakiwepo “
"Najua hali ya hewa inavyokuwa jukwaani tukicheza hapa,Kuna wakati nilikuwa na timu ya Taifa yake Angola tukicheza dhidi ya Morocco Ilikuwa ni vyema sana lakini ndio uhalisia,Tutacheza uwanja ukiwa mtupu”
"Tunawajua wapinzani wetu wana timu nzuri ambayo wanaweza kucheza katika mazingira tofauti ya kimbinu. Tumejiandaa kuwakabili kwa namna yoyote ambayo watakuja nayo.
Hakuna timu bora ambayo haina madhaifu, tutatumia madhaifu yao kupata matokeo. Tuna timu bora ya kupata matokeo katika mazingira magumu" @coachpedrosoaresgoncalves





