pmbet

Kocha wa zamani wa Simba kwenye rada za Esperance de Tunis.

Joyce Shedrack

September 22, 2026
Share :

Kocha wa zamani wa Simba raia wa Hispania Pablo Franco Martín ameibuka kuwa mmoja wa wagombea wanaoongoza kuchukua nafasi ya ukocha wa klabu ya Espérance de Tunis.

Pablo Franco deja el MAS Fés después de guiarle a su primer título de Liga  en 41 años

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, mazungumzo tayari yamefanyika nyuma ya pazia huku viongozi wa klabu hiyo wakitathmini hatua inayofuata katika suala la benchi la ufundi.

 

Franco Martín ana uzoefu katika soka la Afrika Kaskazini, akiwa amewahi kuiongoza Maghreb Fès kutwaa ubingwa wa Morocco Botola Pro msimu uliopita na kuwa kocha bora wa ligi hiyo.

 

Uwezo wake wa kuiongoza Maghreb Fès hadi kwenye ubingwa huo umemfanya kuonekana kama mmoja wa makocha wanaoweza kupewa jukumu la kuiongoza Espérance, huku klabu ikiendelea kufanya tathmini kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho.

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet