Kocha wa zamani wa Yanga kuendelea kutikisa ligi ya Afrika Kusini.
Joyce Shedrack
July 3, 2026
Share :
Klabu ya Sekhukhune United, inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini, imemtangaza rasmi Cedric Kaze, aliyewahi kuwa kocha wa Yanga na kocha msaidizi wa Kaizer Chiefs, kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo.

Kaze, raia wa Burundi, amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele kinachoruhusu kuongezwa kwa miaka miwili zaidi kulingana na makubaliano ya pande zote.





