Kocha, wachezaji United kukatwa mishahara
Sisti Herman
April 24, 2024
Share :
Kocha wa Man Utd Erik ten Hag na wachezaji wake watalazimika kupunguzwa mishahara kama endapo watashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.
United kwasasa ipo nafasi ya 7 baada ya michezo 32 huku ikiwa alama 16 nyuma ya Aston Villa ambao wapo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.
Mholanzi huyo ambaye anaongoza kikosi hicho, yeye na vijana wake kwasasa hawana kiwango bora na kwenye miaktaba yao kuna vipengele vinavyowahitaji mshahara kupunguzwa kwa asilimia 25 wakishindwa kumaliza katika nafasi nne za juu.
Chanzo; TalkSports