Kocha Yanga aelezea walivyonusurika kifo kwenye ndege ya AFCON
Sisti Herman
January 11, 2024
Share :
Kocha wa zamani wa klabu ya Yanga Tom Saintfiet ameelezea namna baadhi ya wachezaji na wafanyakazi wa timu ya taifa ya Gambia anayoiongoza walivyonusurika kifo walipokuwa wakielekea Ivory Coast kwa ajili ya michuano ya AFCON 2023 baada ya kuzimia kwa kukosa hewa ya kutosha kwenye ndege ndogo waliyokuwa wamepanda.
"Sote tungekuwa tumekufa. Sote tulilala ghafla (zimia). Nikiwemo na mimi pia baada ya dakika tisa rubani aliamua kurejea kwa sababu hakukuwa na na oksijeni ya kutosha kwenye ndege. Wachezaji wengine hawakuweza kuzinduka [mpaka] mara baada ya ndege kutua. Alimanusra tupate sumu ya kaboni monoksidi hizo nusu saa nyingine tukiwa angani, sote tungekuwa tumekufa." Kocha huyo aliyeiongoza Yanga mwaka 2012 alipohojiwa na jarida la Nieuwsblad:
Sababu ikiwa ni udogo wa ndege ndio ulisababisha ukosefu wa oksijeni kwa wachezaji, na kulazimika kurejea Gambia baada ya tukio hilo la kutisha ambapo pia taarifa zimeeleza kuwa wachezaji wawili walikuwa kwenye hali ya mbaya.