Kocha Yanga atimuliwa kisa Afcon
Joyce Shedrack
January 24, 2024
Share :
Shirikisho la Soka nchini Gambia limetoa taarifa ya kumuaga na kumshukuru kocha wake Tom Saintfiet raia wa Ubelgiji ambaye amejiuzulu mara baada ya mchezo wake wa mwisho hatua ya makundi AFCON 2023 uliomalizika kwa kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Cameroon.
Matokeo hayo yameifanya Gambia iage mashindano ikiwa haina alama yoyote….ikiwa imefungwa mechi zote tatu kwa kuruhusu magoli saba na kufunga mawili pekee.
Kocha Tom Saintfiet ambaye pia amewahi kuinoa Klabu ya Yanga SC ya Tanzania, amedumu katika timu hiyo ya taifa ya Gambia kwa kipindi cha miaka mitano na nusu akiipeleka AFCON mara mbili mfululizo.
Saintfiet anakuwa kocha wa pili kufutwa kazi kutokana na matokeo mabaya katika mashindano ya Afcon 2023 ikiwa ni hatua tu ya makundi baada ya kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ghana Chris Hughton kufungashiwa virago.
Unadhani Afcon 2023 itaondoka na makocha wangapi ?