Kodak Black adakwa na dawa za kulevya
Eric Buyanza
December 8, 2023
Share :
Mwanamuziki wa hip-hop kutoka nchini Marekani Kodak Black amekamatwa na polisi baada ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine.
'Rapa’ huyu si mara ya kwanza kudakwa na dawa za kulevya, mwaka jana alikutwa akisafirisha dawa hizo aina ya "Oxycodone" zaidi ya vidonge 30. pia 2018 alidakwa kwa mashitaka 7, ikiwemo kumiliki silaha kinyume cha sheria, na kukutwa na bangi.