Kodak Black akataa ushoga na illuminati, asema 'Nataka kufanya muziki tu'
Eric Buyanza
April 13, 2024
Share :
Pamoja na mambo mengi yanayoendelea na kuzungumzwa hivi sasa kuhusu uchafu na mambo ya kishetani yaliyokithiri kwenye tasnia ya burudani nchini Marekani, rapa Kodak Black ameamua kujiweka kando na Illuminati pamoja na ushoga.
Akiongea hivi karibuni Rapa huyo amesema havutiwi hata kidogo na makandokando yanayoendelea kwenye tasnia ya burudani, na kusisitiza kuwa anachotaka kufanya yeye ni muziki tu na si mabalaa mengine.