KODINHI; Kijiji cha ajabu ambacho kila nyumba ina seti ya Mapacha
Eric Buyanza
June 17, 2024
Share :
Huko nchini India kuna kijiji kidogo kiitwacho "Kodinhi" katika jimbo la Kerala.
Ingawa kwa mara ya kwanza utakapofika hapo utakiona kama kijiji cha kawaida kilichozungukwa na miti pamoja na mashamba kibao, lakini utaanza kushangazwa pale utakapoingia kwenye mitaa ya kijiji hicho.
Litakalokushtua ni kuona nyuso zinazofanana kila kona utakayokatiza, hii ni kutokana na wingi wa kushangaza wa mapacha katika kijiji hiki kilichopewa jina la utani (Mji wa Mapacha) kwani karibu kila nyumba katika kijiji hiki ina seti moja ya mapacha.
Katika takwimu za mwaka 2022, idadi ya mapacha katika kijiji hicho ilifikia jozi 400, na kuifanya kuwa jambo la kipekee na la kushangaza duniani.
Baadhi ya wanakijiji wanahusisha kiwango hicho cha mapacha na nguvu za ajabu za maji ya kijiji hicho.
Hakuna maelezo ya kisayansi kwa jambo hili, Madaktari wamekuwa wakijaribu kutatua fumbo hili kwa muda mrefu, lakini hakuna majibu kamili.