Koffi Olomide atua Bongo tayari kukiwasha kesho kwa mkapa.
Joyce Shedrack
June 28, 2024
Share :
Mwanamuziki mkongwe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Koffi Olomide, amewasili kwenye ardhi ya Tanzania kwa ajili ya show itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa.
Msanii huyo ataungana na Harmonize kuwa wasanii wakubwa wawili watakaoshiriki jukwaa moja kwenye show hiyo iliyoandaliwa na moja ya kampuni ya hapa Tanzania kwa kushirikiana na klabu ya Yanga.
Baada ya kuwasili Olomide amesema moja ya kitu kikubwa alichokikumbuka Tanzania ni rafiki zake wa hapa na mashabiki wake ambao kesho ataenda kuwapa burudani.