Kolabo ya Davido na Wizkid ingeukuza zaidi muziki wa Afrobeats
Eric Buyanza
July 9, 2025
Share :
Meneja wa Davido, Asa Asika amedai kuwa muziki wa Afrobeats ungekuwa na mafanikio zaidi kama Davido angeshirikiana na Wizkid.
Asika alitoa kauli hiyo alipokuwa kwenye mahojiano na Podcast ya Afropolitan alipokuwa akizungumzia mafanikio ya muziki wa Afrobeats kimataifa ambapo aliwataka wasanii kutanguliza ushirikiano kwenye kazi zao jambo ambalo litaongeza mvuto wa muziki kimataifa.
"Afrobeat ingekuwa kubwa zaidi kama Davido, Wizkid na wengine wangeshirikiana. Ninaweza kuwa nimekosea lakini kuna uwezekano mkubwa wa Afrobeat kuwa na mafanikio zaidi”