Komasava ya Diamond Platnumz kuwania tuzo ya Grammy.
Joyce Shedrack
October 11, 2024
Share :
Diamond awasilisha ngoma zake katika vipengele viwili vya tuzo za grammy 2024/2025, Vipengele hivyo ni ‘Best music video’ na ‘Best African Music Performance’ kupitia ngoma yake ya ‘Komasava’ wasanii watakaowania tuzo hizi watatangazwa rasmi novemba 8 2024, na ugawaji wa tuzo utafanyika katika ukumbi wa Crypto.Com uliopo mjini Los Angeles Marekani Feb 2, 2025.

Remix Video ya ngoma hiyo iliyopasua mipaka Duniani ilitoka julai 26 mwaka huu Diamond akiwashirikisha wasanii wakubwa akiwemo msanii wa Marekani Jason Derulo na Waafrika Kusini Khalili Harisson pamoja na Chley kwa sasa inawatazamaji zaidi ya milioni 23 kwenye mtandao wa YouTube.





