pmbet

Komasava yatikisa Marekani yazama Billboard.

Joyce Shedrack

August 7, 2024
Share :

Komasava ngoma ya nyota wa bongofleva nchini  Diamond Platnumz inaendelea kufanya vizuri ikiwa ni miezi mitatu tu tangu iachiwe tayari imeandika historia ya kuwa ngoma ya kwanza kutoka Tanzania kuingia kwenye chati za Billboard za Nchini Marekani.

Wimbo huo umeingia kwenye orodha ya Billboard U.S. Afrobeats Songs kwa nyimbo zilizo Top 50 na kushika nafasi ya 39.

 Chati za Billboard zinaorodhesha nyimbo za Afrobeats kutoka Afrika zinazofanya vizuri zaidi nchini Marekani kwenye kila kitu ikiwemo mauzo, downloads, utazamaji wa video na kusikiliza kwenye majukwaa ya muziki.

Wimbo huo ambao video remix yake Diamond alifanya kolabo kwa kumshirikisha Jason Derulo wa Marekani na Waafrika Kusini wawili Khalil Harrison pamoja na Chley tayari imefikisha watazamaji zaidi ya milioni saba YouTube ikiwa ni siku 12 tangu video hiyo iachiwe.

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet