pmbet

Kombora la Ukraine laua 4 Urusi, 120 wajeruhiwa

Eric Buyanza

June 24, 2024
Share :

Watu wanne, wakiwemo watoto wawili, wameuawa kutokana na shambulio la kombora la Ukraine mjini Sevastopol, nchini Urusi huku zaidi ya wengine 120 wakijeruhiwa, taarifa zimeripoti.

Kwa mujibu wa gazeti la Ria Novosti miongoni mwa waliojeruhiwa ni watoto 27 akiwemo binti wa miaka 9 ambaye ni mtoto wa Naibu Meya wa Magadan, Oleg Averyanov ambaye alikuwa na wazazi wake ufukweni wakati shambulio hilo likitokea.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi, imeilaumu Marekani pamoja na Ukraine kwa shambulio hilo lililofanywa kwa kutumia makombora ya masafa marefu ya ATACMS ambayo yalitolewa kwa Ukraine na Marekani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet