Kombora la Urusi latua karibu na msafara wa Zelensky
Eric Buyanza
March 7, 2024
Share :
Shambulio la kutisha la kombora la Urusi katika mji wa bandari wa Odesa wa Ukraine, limeripotiwa kutua karibu na msafara wa Rais Volodymyr Zelensky na waziri mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis.
Waziri mkuu wa Ugiriki aliyekuwa ziarani nchini Ukraine, amelielezea shambulizi hilo kuwa kubwa na la kushutukiza.
Mitsotakis amesema kuwa mwenyeji wake Zelensky alikuwa akimtembeza kwenye bandari ya Odesa, na kisha kusikia mlipuko mkubwa, muda mchache baada ya kuingia kwenye magari ya misafara.
Jeshi la wanamaji la Ukraine limelieleza shirika la habari la AFP kwamba, shambulio hilo dhidi ya miundombinu ya bandari limewaua watu watano na wengine kujeruhiwa.
Urusi na Ukraine zimeongeza mashambulizi ya angani huku wanajeshi wa Moscow wakisonga mbele katika uwanja wa mapambano. Ukraine inakabiliwa na upungufu wa wafanyakazi na silaha.