Kompany kumrithi Tuchel Bayern
Sisti Herman
May 23, 2024
Share :
Klabu ya Bayern Munich ipo kwenye hatua za mwisho kumpata kocha wa klabu ya Burnley ya Uingereza Vicent Kompany kwaajili ya kurithi nafasi ya kocha mkuu iliyoachwa Thomas Tuchel ambaye ameachana na klabu hiyo mara baada ya kutamatika kwa msimu.
Bayern imekamilisha mazungumzo na Kompany na kwa mujibu wa dawati la taarifa za usajili la kituo cha Sky Sport Bayern kwasasa wanaangalia namna ya kumalizana na Burnley ili kumnyakuwa Kompany.