pmbet

Kongo wanayataka mafuvu yao yaliyochukuliwa wakati wa ukoloni

Eric Buyanza

June 25, 2026
Share :

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Judith Suminwa Tuluka, amemwandikia mwenzake wa Ubelgiji, Bart De Wever, kuomba rasmi kurejeshwa kwa mamia ya mafuvu ambayo "yalichukuliwa" wakati wa ukoloni.

 

Mabaki zaidi ya 500 ya binadamu, hasa Wakongo lakini pia Wanyarwanda na Warundi, yanaaminika bado yanahifadhiwa katika taasisi za Ubelgiji.

 

Waziri Mkuu wa Kongo anasisitiza katika barua yake kwamba sampuli zilizohifadhiwa katika Jumba la Makumbusho la Sayansi Asilia huko Brussels ni za wafu ambao "lazima waweze kupumzika kwa heshima katika nchi yao ya asili na hawawezi kuchukuliwa kama vitu vya urithi."

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet