pmbet

Kongo yaishutumu Apple kwa kutumia ''Madini ya Damu''

Eric Buyanza

April 26, 2024
Share :

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeishutumu kampuni ya teknolojia ya mawasiliano ya Apple kwa kutumia madini yaliochimbwa kinyume cha sheria kutoka eneo lake la mashariki kwenye kuunda bidhaa zake. 

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa mawakili wa serikali hiyo wenye makazi yao mjini Paris, Ufaransa, wameitumia kampuni hiyo onyo rasmi la kuitaka isitishe mara moja shughuli hiyo na kuionya kuwa huenda ikachukuliwa hatua za kisheria iwapo itaendelea kufanya hivyo.

Mawakili hao wameishtumu Apple kwa madai ya kununua madini yaliongizwa nchini Rwanda kutoka Kongo kinyume cha sheria ambapo baadaye husafishwa na kuingizwa katika soko la kimataifa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet