pmbet

Kongo yataka Rwanda iwekewe vikwazo, yaituhumu kuwasaidia M23

Eric Buyanza

June 29, 2024
Share :

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Judith Suminwa Tuluka amesema kwamba serikali ya Kinshasa haitaki mazungumzo na Rwanda, kwa sababu inaituhumu kuwasaidia waasi wa kundi la M23 huko mashariki ya nchi yake. 

Alipoitembelea kambi ya wakimbizi karibu na Goma siku ya Alhamis, Tuluka ametoa wito kwa washirika wakuu wa Congo kuchukua hatua kali na vikwazo dhidi ya Kigali.

Hata hivyo VOA imeripoti kuwa siku ya Alhamisi rais wa Angola Joao Lourenco akiwa katika ziara huko Ivory Coast amesema kwamba mazungumzo yananedelea katika kiwango cha mawaziri kwa lengo la kuwaleta pamoja viongozi wa Rwanda na DRC kwa haraka iwezekanavyo ili kukubaliana juu ya kupatikana amani ya kudumu Mashariki ya Congo.

Angola imekua ikijaribu kupatanisha nchi hizo mbili kutokana na ugomvi katika jimbo la kivu ya Kaskazini ambako waasi wa M23 wanadaiwa kuungwa mkono na Rwanda wamekua wakipigana na jeshi la serikali tangu mwishoni mwa 2021.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet