pmbet

Kongo yatangaza mlipuko wa homa ya nyani

Eric Buyanza

April 25, 2024
Share :

Jamhuri ya Kongo imetangaza mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nyani, baada ya visa 19 kuthibitishwa katika miji mitano ikiwa ni pamoja na mji mkuu Brazzaville. 

Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Gilbert Mokoki amesema hakuna vifo vilivyorekodiwa kufikia sasa, lakini ametoa wito kwa umma kuchukua tahadhari, kwa kukaa mbali na wanaoshukiwa kuambukizwa homa hiyo, kuepuka kukaribiana na wanyama na kutoshika nyama za wanyamapori kwa mikono mitupu. 

Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO) homa ya nyani iligunduliwa kwa mara ya kwanza kwa binaadamu katika nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 1970.

Dalili zake zikiwa ni pamoja na homa, maumivu na vidonda kwenye ngozi. 
DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet