pmbet

Kongo yawarejesha makwao wamarekani waliohukumiwa kifo

Eric Buyanza

April 9, 2025
Share :

Wamarekani watatu waliohukumiwa kifo kwa kushiriki jaribio lililoshindwa la mapinduzi nchini Kongo mwaka jana wamerejeshwa makwao nchini Marekani, ikiwa ni siku chache tu baada ya hukumu zao za kifo kubatilishwa na kuwa za maisha.

Msemaji wa rais wa Kongo Tina Salama amesema watu hao watatu watatumikia vifungo vyao nchini Marekani kufuatia kurejeshwa kwao jana Jumanne kulikofanikishwa na Ubalozi wa Marekani. 
Miongoni mwa Wamarekani hao watatu ni Marcel Malanga mwenye umri wa miaka 21 ambaye ni mtoto wa kiongozi wa mapinduzi hayo aliyeuawa marehemu Christian Malanga, Marcel anasema baba yake alimlazimisha kushiriki mapinduzi hayo.

Kurejeshwa huko kumejiri huku kukiwa na juhudi za mamlaka za Kongo kutia saini mkataba wa madini na Marekani ili ipewe msaada wa ulinzi utakaoisaidia Kinshasa kupambana na waasi mashariki mwa nchi hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet