Korea yapiga marufuku ulaji na uuzaji wa nyama ya mbwa
Eric Buyanza
January 9, 2024
Share :
Sheria hiyo ya kupiga marufuku ulaji na biashara ya mbwa kama kitoweo itaanza kutumika rasmi mwaka 2027.
Katika nchi hiyo, ulaji nyama ya mbwa ni jambo la kawaida ambalo wanaharakati kwa muda mrefu wamekuwa wakilipigia kelele wakisema ni kitendo kinachoifedhehesha Korea Kusini kimataifa.
Hatua hii ya kupiga marufuku utamaduni wa kutumia kitoweo hicho, imepata nguvu zaidi chini ya Rais Yoon Suk Yeol ambaye binafsi ni mpenzi wa wanyama na mkewe ni mkosoaji mkubwa wa biashara ya nyama ya mbwa.
Taarifa zinasema kuna wakati nchini humo zaidi ya mbwa milioni moja walichinjwa kwa mwaka kwa ajili ya kitoweo.