Kroos amvulia kofia Bellingham
Sisti Herman
January 23, 2024
Share :
Mchezaji mwandamizi wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani Toni Kroos amesema uwezo wa kufikiria wa kiungo mshambuliaji kinda wa klabu hiyo Jude Bellingham ni wa daraja la juu tofauti na umri wake.
Kroos amechapisha maoni hayo akijibu chapisho la Bellingham kupitia mtandao wa kijamii mara baada ya mchezo dhidi ya Almeria ambapo Bellingham alifunga goli 1 na kutoa pasi moja ya bao kwenye ushindi wa 3-1.
“Akili hii kwa kijana wa miaka 20, ni daraja luu” yalisomeka maoni ya Kroos kwenye chapisho la Bellingham baada ya mchezo huo lililokuwa na maneno “Klabu hii (Madrid), uwanja huu(Santiago Bernabeu, timu hii, ni tofauti”