Kroos aongeza mkataba Madrid hadi 2025
Sisti Herman
March 27, 2024
Share :
Kiungo wa kati wa Real Madrid Toni Kroos amefikia makubaliano ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kusalia kwenye klabu hiyo hadi 2025.
Kroos ambaye alistaafu timu ya taifa mwaka 2021 na kurejea mwaka huu kwenye michezo miwili ya kirafiki na Ujerumani ametoa pasi mbili za mabao na kutandaza soka safi.
Kroos ameshinda kila aina ya taji akiwa na Real Madrid na Bayern Munchen ikiwemo kombe la dunia mara moja akiwa na Ujerumani na Uefa Champions League mara 5.
Chanzo; Fabrizio Romano