Kroos atumia sekunde 7 tu kuwaua Ufaransa baada ya kustaafu
Sisti Herman
March 24, 2024
Share :
Mara baada ya kurejea kwenye timu ya Taifa ya Ujerumani ambayo alistaafu mwaka 2021, kiungo wa Real Madrid Toni Kroos jana alitumia sekunde 7 tu uwanjani kuwajulisha wapinzani wao Ufaransa kuwa yupo uwanjani baada ya kutoa pasi ya goli mara baada ya kuanza kwa mchezo.
Pasi ya Kroos iliwapa goli la utangulizi kati ya mawili waliyoshinda kwa Wafaransa ilivunja mistari ya uzuiaji ya Ufaransa na kumkuta Florian Wirtz wa Bayer Leverkusen nje ya boxi na kupiga shuti liliwatanguliza Wajerumani.
Goli lingine la Ujerumani lilifungwa na kiungo mshambuliaji wa Arsenal, Kai Havertz