pmbet

Kucheza saa 8 mchana Afcon sio unyama - Mane

Sisti Herman

January 16, 2024
Share :

Kinara wa soka wa Senegal, Sadio Mane amesema kuwa michuano ya Afcon 2023 haipaswi kuchezwa mapema majira ya saa nane mchana.

“Kulingana na hali ya joto la juu lenye kuzidi nyuzijoto 30, mechi za kwanza kuchezwa saa nane jua kali si jambo ambalo linapaswa kufanyika katika karne hii” amenukuliwa Mane.

“Ulimwengu unatazama Afcon na iwapo wanataka kuona ubora wa wachezaji hawapaswi kuchezesha mchana” alimaliza Mane alipohojiwa na TRT Afrika.

Kocha wa Gambia amesema hana haja ya kutafuta visingizo kutokana na hali ya hewa kwani kila timu inapambana katika eneo moja na sawa.

Senegali waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Gambia kwenye mechi yao ya kwanza hapo jana Jumatatu katika mji mkuu Yamoussoukro, Ivory Coast.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet