Kudhibiti kufanyiana mitihani, mashine ya kutambua alama za vidole kutumika
Eric Buyanza
July 5, 2024
Share :
Maprofesa wa vyuo vikuu mbalimbali nchini wamependekeza njia za kudhibiti udanganyifu wa mitihani ya elimu za juu.
Kwa mujibu wa mapendekezo hayo wametaka kuwe na mfumo wa kumtambua mtahiniwa kwa alama za vidole kabla ya mtahiniwa kuingia kwenye chumba cha mtihani, ili kuziba mianya ya wanaotoa fedha kufanyiwa mitihani.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania, Prof. Elifasi Bisanda, alikumbushia namna aliowaita mamluki 17 waliokamatwa walivyoingia katika chuo chake siku za karibuni na kuwafanyia mtihani baadhi ya wanafunzi katika chuo hicho akibainisha kuwa walitumia njia ya kughushi vitambulisho.
Maprofesa hao walitoa mapendekezo hayo juzi katika kipindi cha mizani kinachorushwa na TBC kilichokuwa na mada ya ‘Udanganyifu wa mitihani elimu ya juu’.