pmbet

Kudus aifanya Afcon kuvutia

Sisti Herman

January 21, 2024
Share :

Mashindano ya AFCON 2023 yanaendelea kushika kasi nchini Ivory Coast ikiwa kwasasa iko kwenye mzunguko wa pili wa hatua ya makundi na tayari Cape Verde na Senegal zimekata tiketi ya kufuzu hatua ya 16 bora.

 

Miongoni mwa mambo mengi yanayoendelea nchini Ivory Coast, tayari kuna nyota kadhaa waliotikisa na kuzungumzwa zaidi kwenye michuano hiyo.

 

Emilio Nsue nyota wa timu ya Taifa ya Equatorial Guinea ni miongoni mwa nyota wanaozungumzwa zaidi kwasasa baada ya kufunga hattrick [Magoli matatu mechi moja] dhidi ya Guinea Bissau na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hattrick kwenye michuano ya mwaka huu huku akifanya hivyo tangu mwaka 2008 iliposhuhudiwa hattrick kwenye michuano ya AFCON.

 

Mohamed Kudus ni miongoni mwa nyota waliozungumzwa zaidi hadi hivi sasa kutokana na ubora aliouonyesha kwenye mchezo wa Ghana dhidi ya Misri [2-2] akiingia kambani mara mbili [2].

 

Baadhi ya wadau wa soka wanaamini kuwa Kudus ameiongezea thamani michuano hii na kumtaja kama Jay Jay Okocha mpya wa Afrika kutokana na uwezo wake wa kuuchezea mpira.

 

Kocha mkuu wa kikosi cha Ghana Chris Hughton aliweka wazi kuwa ana bahati kuwa na Kudus kwenye kikosi chake.

 

“Nadhani tuna bahati kuwa amekuja kwenye kikosi chetu, kwenye mechi yake ya kwanza ameonyesha uwezo mkubwa sana, alikuwa na kiwango bora kipindi ambacho hatukuwa bora, anacheza vizuri kwa kiwango cha hali ya juu”, alisema kocha Chris.

 

Kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Ghana George Boateng amesema kuwa Kudus katika mchezo wao dhidi ya Misri hakuwa sawa, japo alionyesha uwezo mkubwa sana.

 

“Tunajua nini Mohamed Kudus anaweza kufanya, Mo ni mchezaji mzuri, anaweza kufunga, kutengeneza magoli na ni mchezaji wa timu”.

 

“Kwenye mchezo dhidi ya Misri hakuwa sawa lakini alifanya kila kitu, kwa timu yake na kwa nchi yake”, Alisema kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Ghana George Boateng.

 

Nyota wa timu ya Taifa ya Ghana Daniel Amartey anajivunia uwepo wa Kudus kwenye kikosi hicho kutokana na ubora alionao kwasasa na kusisitiza kuwa akiendelea kujifunza atakuwa bora zaidi.

 

“Ni mchezaji mzuri kwetu, nina furaha kuwa tuna Kudus nchini kwetu, ni mchezaji mzuri, anaweza kufanya vizuri zaidi, mhimu aendelee kujifunza ili awe bora zaidi”, nyota wa Black Stars Daniel Amartey.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet