pmbet

Kuendesha trekta na kulisha ng'ombe ndiyo ndoto yangu - Haaland

Eric Buyanza

July 9, 2026
Share :

Mshambuliaji wa Manchester City na timu ya Taifa ya Norway, Erling Haaland amesema ndoto yake kubwa baada ya kustaafu soka ni kununua shamba, kuendesha trekta, na kulisha ng'ombe.

 

"Nitajaribu kupumzika kadri niwezavyo...kuwa shambani... kuendesha trekta na kulisha ng'ombe wangu, hiyo ndiyo ndoto yangu kubwa na ndivyo ninavyotaka kufanya nitakapostaafu soka" alisema Haaland kwenye mahojiano na SkySports.

 

Haaland alilelewa katika mji wa Bryne nchini Norway, ambao ni mji unaojulikana sana kwa shughuli za kilimo na ufugaji. Tangu udogo wake, amekuwa na mazoea ya kwenda kusaidia kazi kwenye mashamba ya viazi ya ndugu zake.

 

Nyota huyo ameweka wazi kuwa kwenda shambani kumemsaidia sana kupata utulivu wa akili na kumpunguzia shinikizo kubwa linalotokana na umaarufu wa soka. Mara kwa mara amekuwa akipiga picha akiendesha matrekta au akikata kuni wakati wa likizo zake huko Norway.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet