Kufanya mapenzi mara 2 kwa wiki, kutakuepusha na mshtuko wa moyo
Eric Buyanza
March 1, 2024
Share :
Utafiti uliofanyika mwaka 2010 unaonyesha kuwa wanaume wanaofanya mapenzi angalau mara mbili kwa wiki, na wale wanawake wanaoridhishwa kimapenzi wana uwezekano mdogo wa kupata mshtuko wa moyo (Heart Attack).
Faida zinaweza kuwa nyingi: lakini kufanya mapenzi ni aina ya mazoezi ambayo husaidia kuimarisha moyo, kupunguza shinikizo la damu, kupunguza stress, kupunguza hisia za upweke na kuondoa wasiwasi......amesema Michael Blaha, Mkurugenzi wa Tafiti za Kimatibabu katika Taasisi Johns Hopkins Ciccarone iliyopo nchini Marekani.