Kufuatia jeraha la jana, Monaco yavunja mkataba na Pogba
Eric Buyanza
August 12, 2026
Share :

Klabu ya AS Monaco imechukua uamuzi wa kuvunja mkataba na kiungo Paul Pogba kwa makubaliano ya pande zote mbili, ambao ulipaswa kumalizika mwaka 2027.
Uongozi wa klabu hiyo ya Ufaransa umemuarifu rasmi kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 kuwa hayupo tena kwenye mipango yao ya baadae. Pande zote mbili hivi sasa ziko kwenye mazungumzo ya mwisho ili kukamilisha taratibu za malipo ya kifedha kabla ya soko la usajili kufungwa.
Hatua ya kuvunja mkataba inaaminika imekuja baada ya Pogba kupata jeraha kubwa kwenye paja la kushoto jana asubuhi Agosti 11 wakati wa mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya huko St. George's Park nchini Uingereza.
Kiungo huyo alipata jeraha na kupiga kelele za maumivu makali kabla ya kuanguka chini wakati wa mazoezi.





