"Kuhusu Ballon d'or mabao 73 yanajieleza" Harry Kane.
Joyce Shedrack
September 18, 2026
Share :
Mshambuliaji wa Bayern Munich Harry Kane amesema takwimu zake za mabao 73 zinatosha kueleza ubora wa msimu wake huku akizungumzia nafasi yake katika mbio za kuwania tuzo ya Ballon d’Or.
Akizungumza na Marca Kane alisema hataki kuzungumza sana kuhusu mafanikio yake binafsi, akiamini kwamba idadi kubwa ya mabao aliyofunga inajieleza yenyewe.
“Sipendi kuzungumza kuhusu mimi, mafanikio yangu au nafsi yangu kwa sababu mabao 73 yanajieleza yenyewe. Umekuwa msimu wangu bora kwa mbali na takwimu zilikuwa za kushangaza kabisa,” amesema Kane.
Kane amekuwa katika kiwango bora msimu huu, huku akisisitiza kuwa takwimu hizo zinaonyesha mchango wake uwanjani. Kauli yake imekuja wakati jina lake likitajwa katika mjadala kuhusu wagombea wa tuzo ya Ballon d’Or, inayotolewa kwa mchezaji bora wa mwaka.





