Kuilazimisha Iran kujisalimisha ni 'ndoto ya mchana' - Masoud
Eric Buyanza
May 21, 2026
Share :

Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa kijamii wa X, Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, aliandika kuwa kuilazimisha Iran ijisalimishe ni “ndoto ya mchana.”
Rais huyo aliongezea kuwa “Iran imekuwa ikizingatia kwa uaminifu ahadi zake na imetumia kila njia ya kuzuia vita”
“Kuilazimisha Iran kujisalimisha ni ndoto ya mchana, na lazima kuwe na heshima katika njia zote za diplomasia zinazotumika ili kupata amani ya kudumu”
Kauli ya Pezeshkian inajiri wakati Rais wa Marekani Donald Trump,alidokeza kuwa mazungumzo na Iran yako katika hatua za mwisho, na kuonya kuwa mashambulizi zaidi yanaweza kutekelezwa ikiwa Tehran haitakubali kuafikia makubaliano.
BBC





