pmbet

Kuiona Yanga na Mamelod Bure kwa Mkapa

Sisti Herman

March 21, 2024
Share :

Afisa habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga Ali Kamwe leo kupitia mkutano na wanahabari ametangaza viingilio vya mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika kati ya Yanga na Mamelod Sundwons utakaochezwa wiki ijayo.

 

Hizi ni nukuu za Ali Kamwe leo;

 

"Mechi ya Young Africans SC dhidi ya Mamelodi Sundowns itachezwa majira ya saa tatu usiku Tarehe 30 March 2024. Mamelodi wataingia nchini siku ya Tarehe 28 March 2024 majira ya saa moja kamili usiku"

 

"Wote tunakubaliana mechi ya Mamelodi ni mechi kubwa zaidi kwenye robo fainali ya CAFCL msimu huu na Viingilio ni kama vifuatavyo:
𝐕𝐈𝐏 𝐂 𝟏𝟎,𝟎𝟎𝟎
𝐕𝐈𝐏 𝐁 𝟐𝟎,𝟎𝟎𝟎
𝐕𝐈𝐏 𝐀 𝟑𝟎,𝟎𝟎𝟎

Tunafahamu mechi itaisha usiku sana, kwa kuwajali mashabiki wetu na dhamira ya nchi yetu hasa kwenye sekta ya michezo Viongozi wetu wameamua jukwaa la 𝐌𝐙𝐔𝐍𝐆𝐔𝐊𝐎 litakuwa 𝐁𝐔𝐑𝐄.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet