pmbet

Kujitetea kwangu kwa bunduki kulitupa upenyo wa kukimbia - Ole Sendeka

Eric Buyanza

March 30, 2024
Share :

Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amenusurika baada ya wasiofahamika kushambulia gari lake kwa risasi akiwa safarini katika Kijiji cha Ngabolo Wilayani Kiteto, jana Machi 29, 2024.
 

Kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime amesema jeshi la polisi limetuma wataalam wa Matukio yaliyohusisha matumizi ya risasi kutoka Makao Makuu Dodoma imetumwa kwenda kushirikiana na Timu ya Manyara kubaini Wahusika na madhumuni yao au kusudio lao, na baada ya uchunguzi taarifa kamili itatolewa.
 

Akinukuliwa na chombo kimoja cha habari, Ole-Sendeka amesema kitendo chake yeye kuanza kupiga risasi hewani kuwatisha watu waliomvamia na kumfyatulia risasi kilitengeneza upenyo wa yeye na Dereva wake kugeuza gari na kukimbia kutoka eneo la tukio.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet