pmbet

Kukaribisha tu kuaga ahaaa! Simba yalamba 'Thank You' nyingine.

Joyce Shedrack

July 12, 2024
Share :

Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia Moses Phiri ametoa taarifa ya kuwashukuru viongozi wa klabu ya Simba na mashabiki kwa kipindi chote alichokuwa ndani ya timu hiyo.

Phiri amechapisha ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram unaothibisha kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi cha simba kuelekea msimu ujao.

Moses Phiri ameandika....
"Leo ndio mwisho wa mimi kuwa mchezaji wa Simba, shukrani zote ziwaendee wachezaji nilioshirikiana nao, viongozi wa Simba na Rais Mh. Mo Dewji kwa kunifanya kuwa sehemu ya historia ya Simba Ahsante sana..

"Mwisho kwa mashabiki wote wa Simba 😢😢 nawapenda sana, asanteni sana kwa sapoti yenu mlionipa, mtabaki kuwa moyoni mwangu siku zote, tutakutana tena mjini hapo bongo nikifanya biashara".

Taarifa zinasema baada ya mazungumzo ya muda mrefu klabu ya Simba imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na mchezaji huyo ambaye alikuwa Power Dynamos kwa mkopo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet