Kukutana na Chris Brown kulibadilisha maisha yangu - Davido
Eric Buyanza
April 23, 2025
Share :
Kutoka nchini Nigeria, msanii wa muziki wa Afrobeats, Davido, amefichua kuwa staa wa muziki wa R&B kutoka Marekani, Chris Brown amekuwa na mchango mkubwa kwenye kazi yake ya muziki.
Akiongea kwenye 'podcast' ya Bagfuel Brigade, Davido anasema muziki wake ulianza kuinuka kikubwa baada ya kukutana kwa mara ya kwanza na Chris Brown mwaka wa 2018.
"Kukutana na Chris Brown kulibadilisha maisha yangu, nilikutana nae mwaka 2018. Alikuwa na rafiki yake mmoja wa karibu sana wa kiNigeria ambae namjua, yule rafiki alinipigia simu siku moja kwenye Facetime na wimbo wangu ukawa unachezwa kwa nyuma, nikamuuliza yuko wapi akanijibu yuko nyumbani kwa Chris Brown, sikuamimi nikamuuliza unasemaje?
"Alimpa Chris Brown simu, hiyo ilikuwa mara yetu ya kwanza kuongea. Miezi michache baadae nilienda Marekani na kukutana nae. Tangu tukutane kwa mara ya kwanza tukawa marafiki wakubwa."