Kumbe Chama hajawahi kuifunga Yanga kwenye ligi kuu
Sisti Herman
June 24, 2024
Share :
Je wajua, tangu kujiunga kwake na klabu ya Simba Julai 2018 kiungo mshambuliaji Clatous Chota Chama hajawahi kuwafunga hata goli moja mahasimu wao klabu ya Yanga kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara.
Tangu Chama ajiunge na Simba akitokea Lusaka Dynamos, Simba na Yanga wamekutana mara 12 kwenye ligi kuu, Yanga wakishinda mara 4, Simba wakishinda mara 2 na kutoa sare mara 6 huku Chama akiwa hajafunga hata mara moja.
Chama ameifunga Yanga kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho msimu wa 2020/22, Simba wakishinda 4-1.
Chama anahusishwa kuwa kwenye mazungumzo ya kujiunga na Yanga baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Simba.