KUMBE PESA IPO: Arsenal yachanga karata za kumnyakua Haaland
Eric Buyanza
October 3, 2026
Share :

Klabu ya Arsenal imetajwa kuwa miongoni mwa vilabu vichache duniani vyenye uwezo mkubwa wa kifedha unaoruhusu kumsajili mshambuliaji hatari wa Manchester City, Erling Haaland, iwapo nyota huyo ataamua kuondoka.
Hali ya kiuchumi ya Arsenal na usimamizi mzuri wa hesabu za klabu hiyo unawaweka kwenye nafasi nzuri ya kubeba mzigo wa mshahara na ada kubwa ya usajili ya Haaland. Mazungumzo kuhusu mustakabali wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Norway yamepamba moto kufuatia hukumu ya makosa 115 ya kifedha inayoikabili Manchester City, hatua inayoweza kulazimisha mabadiliko makubwa kikosini hapo.
Pamoja na uwezo mkubwa wa kifedha alionao mmiliki wa Arsenal, Stan Kroenke, Arsenal inakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa miamba ya soka ya Hispania. Ripoti kutoka vyanzo vya karibu na mchezaji huyo zinaeleza kuwa Haaland, mwenye umri wa miaka 26, ana ndoto ya kucheza soka nchini Hispania siku zijazo.
Kambi ya Haaland, ikiongozwa na wakala wake Rafaela Pimenta, inaripotiwa kuweka mipango ya muda mrefu ambapo kipaumbele chao kikubwa ni kuhamia Real Madrid au FC Barcelona.





